KENYA-CORONA-AFYA
Coronavirus: Kenya yaendelea kuongoza kwa maambukizi Afrika Mashariki
Imechapishwa:
Idadi ya watu waliombukizwa virusi vya Corona nchini Kenya sasa imefikia zaidi ya Elfu Tano, baada ya watu wengine 254 kuambukizwa siku ya Jumatano na kufikisha idadi hiyo ya 5,206.
Matangazo ya kibiashara
Idadi ya watu waliopoteza maisha sasa imefikia 130. Hali ambayo inawatia wasiwasi, viongozi na raia wa nchi hiyo.
Wagonjwa 1,823 wamepona ugonjwa huo hatari.
Wizara ya afya nchini humo inasema, mji wa Mombasa unasalia kuwa Kaunti hatari kwa maambukizi zaidi ya virusi hivyo.
Kufikia sasa Kenya inaongoza kwa idadi kubwa kubwa ya maambukizi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.