KENYA-CORONA-AFYA

Kenyatta: Kufunguliwa kwa uchumi kunategemea mikakati ya Kaunti katika vita dhidi ya Corona

Rais Uhuru Kenyatta amesema yuko tayari kufungua nchi hiyo iwapo tu serikali hizo za Kaunti zitaweka mikakati ya kupambana na maambukizi mapya
Rais Uhuru Kenyatta amesema yuko tayari kufungua nchi hiyo iwapo tu serikali hizo za Kaunti zitaweka mikakati ya kupambana na maambukizi mapya REUTERS/Njeri Mwangi/

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kufunguliwa tena kwa uchumi wa nchi hiyo kunategemea maandalizi ya serikali za Kaunti 47 kukabiliana na janga la Corona.

Matangazo ya kibiashara

Katika kikao na  Magavana, rais Kenyatta amesema yuko tayari kufungua nchi hiyo iwapo tu serikali hizo za Kaunti zitaweka mikakati ya kupambana na maambukizi mapya ikiwa ni pamoja na kutenga vitanda Elfu 30 katika kila Kaunti kuwatibu wagonjwa wa Corona.

Kenya kwa sasa ina wagonjwa zaidi ya Elfu Tano walioambukizwa virusi vya Corona.

Wizara ya afya nchini humo inasema, mji wa Mombasa unasalia kuwa Kaunti hatari kwa maambukizi zaidi ya virusi hivyo.

Kufikia sasa Kenya inaongoza kwa idadi kubwa kubwa ya maambukizi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.