KENYA-CORONA-UTALII-UCHUMI

Sekta ya utalii Kenya yaathirika pakubwa kutokana na Corona

Waziri wa Utalii Najib Balala amesema kutokana na janga la Corona duniani, na mwenendo wa mamabukizi hayo, watalii kutoka mataifa ya bara Ulaya na kwingineko duniani wanatarajiwa kuanza kuzuru nchi hiyo kuanzia mwaka ujao.
Waziri wa Utalii Najib Balala amesema kutokana na janga la Corona duniani, na mwenendo wa mamabukizi hayo, watalii kutoka mataifa ya bara Ulaya na kwingineko duniani wanatarajiwa kuanza kuzuru nchi hiyo kuanzia mwaka ujao. an Diego Zoo Global via REUTERS

Serikali ya Kenya inasema sekta ya utalii nchini humo imepoteza Mabilioni ya fedha za nchi hiyo tangu kuripotiwa kwa maambukizi ya virusi vya Corona wakati huu idadi ya watu waliombukizwa ikiongezeka na kufikia 6,190 baada ya watu wengine 120 kupatikana na virusi hivyo siku ya Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Wakati serikali nchini humo inapoendelea kutafakari kufungua uchumi wa nchi hiyo na kuwaruhusu watu kuanza kutembea kutoka kaunti moja kwenda nyingine, wadau wa utalii sasa wanasema wanategemea watalii wa ndani na wale kutoka nchi jirani kusaidia kuinua sekta hiyo ambayo imepata hasara kubwa.

Waziri wa Utalii Najib Balala amesema kutokana na janga la Corona duniani, na mwenendo wa maabukizi hayo, watalii kutoka mataifa ya bara Ulaya na kwingineko duniani wanatarajiwa kuanza kuzuru nchi hiyo kuanzia mwaka ujao.

Nchini Kenya, hoteli na migahawa imeruhusiwa kufunguliwa lakini hoteli za kitalii zimebaki tupu kwa kukosa wageni, huku wafanyikazi wakipoteza kazi zao.

Kenya ni miongoni mwa mataifa ya bara Afrika yenye vivutio vingi vya utalii, lakini kutokana na janga la Corona, imefunga anga lake, huku matumaini sasa yakiwa ni kwa watalii wa ndani na wale kutoka nchi jirani.