KENYA-CORONA-AFYA

Kenya kufungua tena mipaka yake Agosti 1

Rais Kenyatta amesema "safari za ndege za kimataifa za kuingia na kutoka nchini Kenya zitarejea Agosti Mosi 2020.
Rais Kenyatta amesema "safari za ndege za kimataifa za kuingia na kutoka nchini Kenya zitarejea Agosti Mosi 2020. REUTERS/Presidential Press Service/Handout

Kenya itaanza tena safari za ndege za kimataifa na za ndani ifikapo Agosti 1 kama sehemu ya kuondoa hatua kwa hatua masharti ya kupambana dhidi ya janga la Corona, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza leo Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

"Safari za ndege ndani na nje ya Kenya zitaanza tena ifikapo Agosti 1," Rais Kenyatta amesema katika hotuba iliyorushwa hewani kwenye runinga ya taifa.

Wakati huo huo Rais wa Kenyatta ameondoa masharti ya usafiri wa kuingia na kutoka katika miji ya Nairobi, Mombasa na Mandera kaskazini mwa nchi.

Akizungumzia kuhusu mwenendo wa maambukizi ya virusi vya Corona, rais Kenyatta amesema hatua ya kufungua miji hiyo mitatu 'inawaweka Wakenya' katika hali hatari na hivyo basi 'naomba tuwe waangalifu'.

Rais Kenyatta pia ametangaza kufunguliwa kwa maeneo ya kuabudu htua kwa hatua kwa kuzingatia muongozo wa kuzuia maambukizi ya Corona uliowekwa na Wizara ya Afya.

Hata hivyo amebaini kwamba makanisa yatafunguliwa baada ya wiki tatu, huku akiwataka viongozi wa kidini kufanya mashauriano kabla ya muda huo kukamilika.