KENYA-CORONA-AFYA-ELIMU

Shule za msingi na Sekondari kufunguliwa mwaka 2021 Kenya

enya kwa sasa ina maambukizi 8,250 na kufikia sasa imerekodi vifo 164 vinavyohusiana na ugonjwa aw Covid-19.
enya kwa sasa ina maambukizi 8,250 na kufikia sasa imerekodi vifo 164 vinavyohusiana na ugonjwa aw Covid-19. REUTERS/Baz Ratner

Serikali ya Kenya imetangaza kuwa, Shule zote za msingi na Sekondari zitafunguliwa mwaka 2021 na wala sio Septemba mwaka huu ilivyokuwa imepangwa, kutokana na ongezeko la visa vya maambukizi ya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Elimu nchini humo Profesa George Magoha amesema wanafunzi watasalia katika madarasa yao ya sasa mwaka ujao.Mwaka huu hakutakuwa na mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne.

Hata hivyo, masomo katika Vyuo Vikuu na taasisi nyingine za elimu ya juu, yanatarajiwa kurejelewa kuanzia mwezi Septemba.

Tangazo hili limekuja baada ya rais Uhuru Kenyatta kufungua nchi hiyo huku akiwataka raia wa nchi hiyo kuchukua tahadhari.

Kenya kwa sasa ina maambukizi 8,250 na kufikia sasa imerekodi vifo 164 vinavyohusiana na ugonjwa aw Covid-19. Wagonjwa 2,414 wamepona ugonjwa huo, wakati visa vya maambukizi na vifo vinaendelea kuongezeka duniani.