KENYA-CORONA-AFYA

Kenya yatangaza hatua mpya za usafiri kudhibiti Corona

Serikali ya Kenya iliondoa marufuku ya kusalia nyumbani Julai 6, 2020.
Serikali ya Kenya iliondoa marufuku ya kusalia nyumbani Julai 6, 2020. SIMON MAINA / AFP

Abiria wa Kimataifa watakaokuja nchini Kenya kuanzia tarehe 1 mwezi Agosti wakati safari za Kimataifa zitakapofunguliwa, hawatawekwa karatini kwa hofu ya kuchunguzwa iwapo wana virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Uchukuzi nchini humo James Macharia ametangaza kanuni za kusafiri nchini humo na kusema abiria wote watakaowasili watapimwa joto na kuchunguzwa iwapo hawana dalili za virusi vya Corona kabla ya kuruhusiwa kuondoka katika uwanja wa ndege.

Kenya inaendelea kushuhudia ongezeko la maambuizi hayo ambayo wiki hii yamefikia Elfu Nane, wakati huu ambao pia nchi hiyo imefunguliwa kwa watu kusafiri.

Kenya itaanza tena safari za ndege za kimataifa na za ndani ifikapo Agosti 1 kama sehemu ya kuondoa hatua kwa hatua masharti ya kupambana dhidi ya janga la Corona, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alitangaza mapema wiki hii.

Pia Rais wa Kenyatta aliondoa masharti ya usafiri wa kuingia na kutoka katika miji ya Nairobi, Mombasa na Mandera kaskazini mwa nchi hiyo.