KENYA-CORONA-AFYA

Kenya yaendelea kuripoti visa zaidi vya Corona

Awali Wizara ya Afya ya Kenya ilikuwa imebashiri kuwa idadi hii ya maambukizi ingetokea mwezi Aprili lakini, inasema haikuwa hivyo kutokana na jitihada za kuzuia maambukizi hayo.
Awali Wizara ya Afya ya Kenya ilikuwa imebashiri kuwa idadi hii ya maambukizi ingetokea mwezi Aprili lakini, inasema haikuwa hivyo kutokana na jitihada za kuzuia maambukizi hayo. Patrick Meinhardt / AFP

Kenya imeripoti vifo 12 vya maambukizi ya virusi vya Corona kwa muda wa saa 24 zilizopita na kuwa na idadi kubwa zaidi ya vifo vilivyowahi kuripotiwa nchini humo kwa siku moja tangu kuzuka kwa janga hilo mwezi Machi na sasa kufikisha idadi ya watu waliopoteza maisha kufikia 197.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya maambukizi imefikia 10,294 baada ya watu wengine 189 kuambukizwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema kwa sasa Wakenya wengi wanaamini kuna maambukizi hayo katika jamii.

Awali Wizara ya Afya ilikuwa imebashiri kuwa idadi hii ya maambukizi ingetokea mwezi Aprili lakini, inasema haikuwa hivyo kutokana na jitihada za kuzuia maambukizi hayo.

Idadi hiyo imeongezeka wakati huu nchi hiyo ikiwa imefunguwa safari za ndani za ndege zikitarajiwa kuanza siku ya Jumatano wiki hii, lakini pia kufunguliwa kwa maeneo ya kuabudu.

Waziri wa Afya nchini humo Mutahi Kagwe akizungumza hivi karibuni, alisisitiza kuwa jukumu la kujilinda dhidi ya maambukizi hayo sasa lipo mikononi mwa Wakenya wenyewe.