SUDANI-KUSINI-IGAD-SIASA-USALAMA

IGAD yawataka viongozi wa Sudani Kusini kuhakikisha amani ya kudumu imepatikana

Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) na makamu wake mpya, kiongozi wa zamani wa waasi Riek Machar (kulia) huko Juba, Februari 20, 2020 wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) na makamu wake mpya, kiongozi wa zamani wa waasi Riek Machar (kulia) huko Juba, Februari 20, 2020 wakati wa mkutano na waandishi wa habari. REUTERS/Jok Solomun

Nchini Sudan Kusini harakati zinaendelea za kuhakikisha mkataba mpya wa amani uliotiwa saini mwezi Septemba mwaka jana huko Addis Ababa Ethiopia unatekelezwa kikamilifu ili kila mtu aweze kushiriki na hatimaye amani ya kudumu na endelevu iweze kupatikana kwenye taifa hilo changa.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi kutoka Mataifa ya IGAD, wamewataka viongozi wanaongoza serikali ya mpito nchini Sudan Kusini, kutekeleza kikamilifu mkataba wa amani.

Wakikutana kupitia mfumo wa video, viongozi hao wamesema utekelezwaji huo ni muhimu sana kwa ajili ya usalama na amani ya ukanda wa IGAD.

Pande hasimu zimekuwa zikivutana kuhusu namna ya kutekeleza baadhi ya vipengele vya mkataba wenyewe, likiwemo suala tata la usalama wa Riek Machar mjini Juba na uundwaji wa jeshi la kitaifa.

Pande mbili hizo hasimu nchini Sudan Kusini zimehusika katika mauaji ya ulipizaji kisasi ambayo yaliibua miganyiko ya kikabila. Makumi ya maelfu ya watu wameuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi kufuatia machafuko hayo.

Serikali ya mpito nchini Sudan Kusini inaongozwa na rais Salva Kii na Makamu wake wa kwanza Riek Machar.

Mawaziri wa serikali mpya ya Sudani Kusini wakila kiapo, huko Juba, Machi 16, 2020.
Mawaziri wa serikali mpya ya Sudani Kusini wakila kiapo, huko Juba, Machi 16, 2020. REUTERS/Jok Solomun