KENYA-CORONA-AFYA-UCHUMI

Safari za ndani za ndege kuanza Kenya

Hivi karibuni Waziri wa Uchukuzi nchini humo James Macharia alitangaza kanuni za kusafiri nchini humo na kusema abiria wote watakaowasili watapimwa joto na kuchunguzwa iwapo hawana dalili za virusi vya Corona.
Hivi karibuni Waziri wa Uchukuzi nchini humo James Macharia alitangaza kanuni za kusafiri nchini humo na kusema abiria wote watakaowasili watapimwa joto na kuchunguzwa iwapo hawana dalili za virusi vya Corona. REUTERS/Baz Ratner

Safari za ndege nchini Kenya zinaanza tena leo kati ya miji ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki, licha ya ongezeko la virusi vya maambukizi ya Corona, ambayo wiki hii yamefikia zaidi ya Elfu 10.

Matangazo ya kibiashara

Safari za kimataifa zinatarajiwa kuanza Agosti 1. Abiria wa Kimataifa watakaokuja nchini Kenya kuanzia tarehe 1 mwezi Agosti wakati safari za kimataifa zitakapofunguliwa, hawatawekwa karatini kwa hofu ya kuchunguzwa iwapo wana virusi vya Corona.

Wakati huo huo, usafiri kutoka jiji kuu Nairobi kwenda maeneo mengine umeshika kasi kwa mujibu wa mwandishi wetu Hillary Ingati aliyetembelea kituo cha mabasi cha Machakos jijini Nairobi.

Hivi karibuni Waziri wa Uchukuzi nchini humo James Macharia alitangaza kanuni za kusafiri nchini humo na kusema abiria wote watakaowasili watapimwa joto na kuchunguzwa iwapo hawana dalili za virusi vya Corona kabla ya kuruhusiwa kuondoka katika uwanja wa ndege.

Waziri wa Afya nchini humo Mutahi Kagwe akizungumza hivi karibuni, alisisitiza kuwa jukumu la kujilinda dhidi ya maambukizi hayo sasa lipo mikononi mwa Wakenya wenyewe.