BURUNDI-UN-SIASA-USALAMA

Umoja wa Mataifa waitaka Burundi kufunguwa ukurasa mpya

Moja ya maeneo ya mji mkuu wa kiuchumi wa Burundi, Bujumbura.
Moja ya maeneo ya mji mkuu wa kiuchumi wa Burundi, Bujumbura. © AFP/Carl de Souza

Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa umeitolea wito serikali mpya ya Burundi 'kufunga ukurasa wa machafuko nchini humo na kufungua ukurasa mpya' na kushirikiana na Umoja wa Mataifa.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, makamishna wa Umoja wa Mataifa, ambao ripoti yao ya mwisho itachapishwa mnamo mwezi Septemba, wametoa wito kwa Rais mpya wa Burundi, Évariste Ndayishimiye, kuonyesha "nia yake ya mabadiliko kwa kushirikiana kikamilifu" na mifumo ya kimataifa ya haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na Tume, na kufungua tena ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu nchini Burundi.

Doudou Diène, mwenyekiti wa tume inayohusika na uchunguzi wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanywa nchini Burundi tangu kuzuka kwa mzozo wa mwaka 2015, amebaini kwamba nchi hiyo sasa iko njia panda.

"Burundi iko kwenye hatua ya kihistoria baada ya kifo cha rais Nkurunziza," amesema kwenye katika mahojiano na mwandishi wetu Esdras Ndikumana. Kuna mabadiliko ya utawala, ya kiongozi kwenye uongozi wa nchi. Tunasema, na nadhani hata jamii ya kimataifa inasema hivyo, kwamba haya ni mageuzi ya kihistoria na kwamba kuna uwezekano wa kuleta mabadiliko au kuzidisha machafuko. "

"Katika hali hii, jamii ya kimataifa inapaswa kuzingatia kwamba mabadiliko rahisi ya mtu hupelekea mabadiliko ya ubora katika uheshimishwaji wa haki za binadamu na demokrasia. Tunatoa wito wa kuwa waangalifu ili kufuatilia hali ya haki za binadamu nchini Burundi. Kuna mambo matatu ambayo yanasababisha hali kuwa mbaya zaidi: mazingira ya ukosefu wa usalama wa kijamii na kisiasa, miundo dhaifu ya serikali, hususan mfumo wa mahakama, na hali ya ukosefu wa usalama kwa ujumla kwa vitendo cya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu vya hivi karibuni na vya zamani, " ameoongeza Doudou Diène, mwenyekiti wa tume inayohusika na uchunguzi wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanywa nchini Burundi tangu kuzuka kwa mzozo wa mwaka 2015.