KENYA-CORONA-AFYA

Wahudumu wa afya 450 waambukizwa Corona, wanne wapoteza maisha Kenya

Awali Wizara ya Afya ilikuwa imebashiri kuwa idadi hii ya maambukizi ingetokea mwezi Aprili lakini, inasema haikuwa hivyo kutokana na jitihada za kuzuia maambukizi hayo.
Awali Wizara ya Afya ilikuwa imebashiri kuwa idadi hii ya maambukizi ingetokea mwezi Aprili lakini, inasema haikuwa hivyo kutokana na jitihada za kuzuia maambukizi hayo. AFP / LUIS TATO

Wizara ya afya nchini Kenya inasema wahudumu wanne wa afya wamepoteza maisha kutokana na janga la Corona huku wengine 450 wakiambukizwa tangu kuripotiwa  kwa kisa cha kwanza mwezi Machi, wakati huu idadi ya maambukizi ikiongezeka na kufikia zaidi ya Elfu 11.

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema Wakenya wengi wanaamini kuna maambukizi hayo katika jamii.

Awali Wizara ya Afya ilikuwa imebashiri kuwa idadi hii ya maambukizi ingetokea mwezi Aprili lakini, inasema haikuwa hivyo kutokana na jitihada za kuzuia maambukizi hayo.

Idadi hiyo imeongezeka wakati huu nchi hiyo ikiwa imefunguwa safari za ndani za ndege ambazo zilianza siku ya Jumatano wiki hii, lakini pia kufunguliwa kwa maeneo ya kuabudu.

Waziri wa Afya nchini humo Mutahi Kagwe akizungumza hivi karibuni, alisisitiza kuwa jukumu la kujilinda dhidi ya maambukizi hayo sasa lipo mikononi mwa Wakenya wenyewe.

Katika hatua nyingine, huko Mombasa mji ulio pwani ya nchi hiyo, wanaharakati wanaopambana na dawa za kulevya wanahofia ongezeko la matumizi ya dawa hizo katika kipindi hiki cha janga la Corona.