KENYA-CORONA-AFYA

Wagonjwa 570 wa Corona wathibitishwa kupona Kenya

Kenya imeripoti idadi kubwa ya watu waliopona virusi vya Corona kwa muda wa saa 24 zilizopita. Hata hivyo idadi ya maambukizi inaendelea kuongezeka katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Afisa wa afya katika manispaa ya jiji la Nairobi akinyunyuzia dawa dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona katika eneo la Kawangware jijini Nairobi, Kenya, Mei 2, 2020.
Afisa wa afya katika manispaa ya jiji la Nairobi akinyunyuzia dawa dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona katika eneo la Kawangware jijini Nairobi, Kenya, Mei 2, 2020. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Afya nchini humo imesema watu 570 wameruhisiwa kutoka hospitalini  na kufikisha idadi ya waliopoana kufikia 3,638.

Katika hatua nyingine, watu wengine 421 wameambukizwa virusi vya Corona na kufanya idadi ya maambukizi kufikia zaidi ya Elfu 11 na mia sita, huku idadi ya vifo ikiwa 217.

Wikki hii wizara ya afya nchini Kenya ilisema wahudumu wanne wa afya wamepoteza maisha kutokana na janga la Corona, huku wengine 450 wakiambukizwa tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza mwezi Machi.

Hivi karibuni Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema Wakenya wengi wanaamini kuna maambukizi hayo katika jamii.

Awali Wizara ya Afya ilikuwa imebashiri kuwa idadi hii ya maambukizi ingetokea mwezi Aprili lakini, inasema haikuwa hivyo kutokana na jitihada za kuzuia maambukizi hayo.

Idadi hiyo imeongezeka wakati huu nchi hiyo ikiwa imefunguwa safari za ndani za ndege ambazo zilianza siku ya Jumatano wiki hii, lakini pia kufunguliwa kwa maeneo ya kuabudu.

Waziri wa Afya nchini humo Mutahi Kagwe akizungumza hivi karibuni, alisisitiza kuwa jukumu la kujilinda dhidi ya maambukizi hayo sasa lipo mikononi mwa Wakenya wenyewe.