Wanawake wapambana kutafuta nafasi kwenye taasisi za uongozi wa nchi Tanzania
Kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba nchini Tanzania, aliyewahi kuza Waziri wa Mambo ya nje nchini humo Bernard Membe amehamia chama cha upinzani cha ACT Wazalendo, baada ya kujiondoa kwenye chama tawala CCM na sasa anatarajiwa kuwania urais kupitia chama hicho.
Imechapishwa:
Bernard Membe amevitaka vyama vya upinzani nchini humo kuungana ili kupata ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.
Katika hatua nyingine, wakati joto la uchaguzi likiongezeka nchini humo, wanawake wameonesha mwamko mkubwa wa kuomba ridhaa kutoka vyama mbalimbali kuchaguliwa kuwania nyadhifa mbalimbali.
Nchini Tanzania wanawake wanafursa ya kuwania Ubunge ama Udiwani kwa namna mbili, mosi kupitia viti maalum pili kujitosa kupambana ili kuchaguliwa na wananchi.
Baadhi ya maeneo wanawake wamechuana na wanaume na kushinda na hivyo kuteuliwa.
Hawa Ghasia ni waziri wa zamani nchini Tanzania, sasa ameomba kuteuliwa na chama chake anasema demokrasia imeshamiri.
Mkurugenzi mtendaji wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Anna Henga, amewapongeza wanawake na kusema sasa wanawake wametambua haki zao
Kwa Mujibu wa katiba ya Tanzania, Wabunge wanawake wanatakiwa kufikia asilimia 30