KENYA-HAKI

Waathiriwa wa sumu ya Lead kutoka mtaa wa Owino Uhuru kulipwa Dola Milioni 12 kama fidia

Wanaharakati wa mazingira nchini Kenya, wameshinda kesi ya wakazi wa mtaa duni wa Owino Uhuru mjini Mombasa, walioathiriwa na sumu kutoka katika kiwanda cha kutengeza madini aina ya Lead.

Mji wa Mombasa, nchini Kenya. (Picha ya kumbukumbu)
Mji wa Mombasa, nchini Kenya. (Picha ya kumbukumbu) CC BY-SA 4.0/wikimedia commons/Leo Hempstone
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa watu waliofurahia uamuzi huu wa Mahakama, ni Phyllis Omido, ambaye mtoto wake alipata tatizo la kiafya kutoka kwenye kampuni hiyo ya kutenengeneza vyuma.

Baada ya kuajiriwa na kampuni hiyo iliofunguliwa mwaka 2008, karibu na makazi ya watu, mtoto wake aliuumia na Madaktari wakathibitisha kuwa alikuwa ameathirika na sumu ya Lead.

Hali hii ilimfanya aanze kufanya utafiti katika mtaa wake na akabaini kuwa, watu wengi walikuwa wanaumwa kama mwanaye na hapo ndipo walipoungana na shirika moja la kiraia kuanza kutafuta haki.

Baada ya maandamano ya wanaharakati na wakazi waliokuwa wanaishi karibu na kampuni hiyo mwaka 2014, kampuni hiyo ilifungwa, huku madai ya kutaka fidia yakiendelea kisha akatuzwa mshindi wa uhifadhi mazingira ya Golden prize.

Baada ya shinikizo la miaka mitano, Mahakama imeagiza walioathiriwa wote walipwe Dola Milioni 12, ambao ni ushindi kwa wakazi wa mtaa wa Owino Uhuru na wanaharakati ambao wanasema ni ushindi kwa waliothirika na kupoteza maisha kutokana na sumu hiyo.