TANZANIA-CORONA-AFYA

John Pombe Magufuli: Tanzania haina tena virusi vya Corona

Mapema mwezi Mei Shirika la Afya Duniani WHO lilikanusha madai ya Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kwamba vipimo vya virusi vya Corona vina hitilafu.
Mapema mwezi Mei Shirika la Afya Duniani WHO lilikanusha madai ya Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kwamba vipimo vya virusi vya Corona vina hitilafu. REUTERS/Thomas Mukoya/File Photo

Rais wa Tanzania John Magufuli amesema nchi hiyo haina tena virusi vya Corona. Kauli ya Magufuli inakuja baada ya Shirika la Afya Duniani kukosoa msimamo wa serikali ya nchi hiyo kwa nanma inavyoshughulikia mapambano dhidi ya janga la Corona.

Matangazo ya kibiashara

Rais Magufuli ameongeza kuwa watu wameshaanza kufahamu ukweli ndio sababu watalii wanakuja katika taifa hilo.

Tanzania iliacha kutangaza idadi ya maambukizi ya virusi hivyo mwezi Aprili, baada ya maafisa wa maabara ya taifa kutuhumiwa kutoa matokeo yasiyo sahihi.

Mapema mwezi Mei Shirika la Afya Duniani WHO lilikanusha madai ya Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kwamba vipimo vya virusi vya Corona vina hitilafu.

Katika mkutano na waandishi wa habari, mkurugenzi wa WHO barani Afrika Matshidiso Moeti alisema "tuna uhakika kwamba hakukuwepo na virusi hivyo awali katika vipimo, hatukubaliani na mtazamo wa Magufuli."

Kauli hii ya WHO ilikuja baada ya Rais Magufuli kusema kwamba vipimo hivyo vina hitilafu baada ya kuonyesha maambukizi ya Corona katika majimaji ya tunda la papai na mbuzi.

Ubalozi wa Marekani miezi kadhaa iliyopita, ulionya kuwa kuna maambukizi makubwa jijini Dar es salaam, madai ambayo serikali nchini humo ilikanusha.