KENYA-CORONA-AFYA

Rais wa Kenya kukutana na magavana wakati corona yaendelea kusababisha majanga

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameitisha kikao cha dharura kisichokuwa cha kawaida na Magavana wa taifa hilo, kujadili ongezeko la virusi vya Corona baada ya kuanza kulegezwa kwa masharti ya watu kutembea, wiki mbili zilizopita.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, atarajia kujadili na wakuu wa majimbo kuhusu Corona ambayo inaendelea kusababisha athari katika sekta mbalimbali nchini humo
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, atarajia kujadili na wakuu wa majimbo kuhusu Corona ambayo inaendelea kusababisha athari katika sekta mbalimbali nchini humo Kenya Govt
Matangazo ya kibiashara

Tangu nchi hiyo kuanza kurejelea hali ya kawaida kwa hatua, maambukizi mapya Elfu saba yameripotiwa pamoja na vifo zaidi ya 80 katika kipindi hicho.

Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, baada ya kuripotiwa kwa kisa cha maambukizi katika Ikulu ya Nairobi tarehe 15 mwezi Juni, amehamishia kazi zake katika Jumba la Harambee liliko na Ofisi yake, katikati ya jiji la Nairobi.

Wasaidizi wa rais Kenyatta ambaye kwa sasa anaishi katika makaazi yake ya kibinafasi wamepunguzwa hasa wazee, lakini wafanyakazi wa Ikulu hawaruhusiwi kuondoka katika eneo hilo na yeyote anayekutana na rais, lazima apimwe.

Mikutano yote mikubwa kwa sasa inafanyika katika jumba la KICC jijini Nairobi.

Kenya kwa sasa ina maambukizi Elfu 13. Siku ya Jumatatu visa vingine 418 viliripotiwa nchini humo.