UGANDA-CORONA-AFYA

Uganda yachukuwa hatua ya kulegeza masharti wakati idadi ya maambukizi yaendelea kuongezeka duniani

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni. Capture d'écran al-Jazeera

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amelegeza masharti zaidi wakati huu taifa hilo linapoendelea kupambana na janga la virusi vya Corona, ambapo watu zaidi ya Elfu moja wamemabukizwa na hakuna mgonjwa aliyefariki dunia.

Matangazo ya kibiashara

Maduka ya jumla yamefunguliwa tena, usafiri wa bodaboda umerejeshwa kwa asilimia kubwa, huku raia wakitakiwa kuvalia barakoa kila wakati wanapokuwa katika maeneo ya umma, lakini masharti ya watu kutotembea kati ya saa tatu usiku hadi saa 11 na nusu asubuhi, yameongezwa.

Kufikia sasa idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona duniani imefikia Milioni 14.9, huku ugonjwa huo ukiwa umesababisha vifo vya watu 616,000. Wagonjwa Milioni 8.43 wamepona ugonjwa huo hatari.

Uganda imejiunga na mataifa mengine barani Afrika na nchi zingine duniani kwa kulegeza masharti , huku shirika la Afya Dunia, WHO, likionya kuhusu kuongezeka kwa maambukizi zaidi, baadaya nchi kadhaa kulegeza masharti.