KENYA-CORONA-AFYA

Kenya: Wagonjwa wa maradhi sugu ndio huathirika zaidi na Corona

Afisa wa afya akinyunyuzia dawa kwenye moja ya mitaa ya Nairobi, Mei 15, 2020 (picha ya kumbukumbu)
Afisa wa afya akinyunyuzia dawa kwenye moja ya mitaa ya Nairobi, Mei 15, 2020 (picha ya kumbukumbu) REUTERS/Njeri Mwangi

Wizara ya Afya nchini Kenya inasema idadi kubwa ya watu wanaopoteza maisha kutokana na virusi vya Corona, wanasumbuliwa na shinikizo la damu, kisukari, saratani na virusi vya Ukimwi.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano watu wengine 10 walipoteza maisha baada ya kuambukizwa virusi vya Corona huku watu wengine 637 wakiambukizwa saa 24 zilizopita na kufikisha idadi nchini humo kufikia zaidia ya Elfu 14 na Mia Nane.

Katibu katika Wizara hiyo Rashid Aman amewaonya watu wanaopuuzia maelekezo ya kujikinga.

Siku ya Jumatatu wiki ijayo, rais Uhuru Kenyatta atakutana na Magavana kutathmini mwenendo wa maambukizi hayo baada ya kufunguliwa kwa mipaka ya Kaunti mbalimbali.

Hayo yanajiriwakati Shirika la Afya Duniani, WHO, na kituo cha udhibiti wa magonjwa barani Afrika, CDC, yameanzisha juhudi kuangalia uwezekano wa madawa ya mitishamba katika kupambana na janga la virusi vya Corona.

Wakati huo huo visa vya maambukizi vilivyoothibitishwa barani Afrika vimekaribia kufika 750,000, zaidi ya nusu vikiorodheshwa nchini Afrika Kusini.