UGANDA-CORONA-AFYA

Kifo cha kwanza kutokana na Corona chathibitishwa Uganda

Wizara ya afya nchini Uganda imetangaza kutokea kwa kifo cha kwanza kinachotokana na virusi vya Corona, siku chache baada ya serikali ya nchi hiyo kuchukuwa hatua ya kulegeza masharti wakati idadi ya maambukizi ikiendelea kuongezeka duniani.

Kifo hicho kimetokea nchini Uganda baada ya nchi hiyo kuanza kulegeza masharti ya watu kuanza kurejelea shughuli zao wa kila siku.
Kifo hicho kimetokea nchini Uganda baada ya nchi hiyo kuanza kulegeza masharti ya watu kuanza kurejelea shughuli zao wa kila siku. REUTERS/James Akena/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Nchi hiyo ya Afrika Mashariki ambayo ina maambukizi zaidi ya Elfu Moja, na Sabini, ilikuwa haijaripoti kifo hata kimoja cha maambukizi hayo baada ya kuzuka kwa virusi hivyo mwezi Machi.

Kifo hicho kimetokea baada ya nchi hiyo kuanza kulegeza masharti ya watu kuanza kurejelea shughuli zao wa kila siku.

Uganda imejiunga na mataifa mengine barani Afrika na nchi zingine duniani kwa kulegeza masharti , huku shirika la Afya Dunia, WHO, likionya kuhusu kuongezeka kwa maambukizi zaidi, baada ya nchi kadhaa kulegeza masharti.

Kufikia sasa idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona duniani imefikia Milioni 15,4 baada ya visa vipya 247,000 kuthibitishwa, huku ugonjwa huo ukiwa umesababisha vifo vya watu 632,000, baada ya vifo 7 096 kuripotiwa. Wagonjwa Milioni 8.76 wamepona ugonjwa huo hatari.