KENYA-CORONA-AFYA

Msemaji wa serikali ya Kenya Cyrus Oguna akutwa na virusi vya Corona

Msemaji wa serikali ya Kenya Cyrus O. Oguna.
Msemaji wa serikali ya Kenya Cyrus O. Oguna. Spokesperson GoK:twitter.com

Msemaji wa serikali ya Kenya Cyrus Oguna amethibitisha kuwa na virusi vya Corona baada ya kufanya vipimo na kupatikana na virusi hivyo.

Matangazo ya kibiashara

Oguna aliwasihi wananchi wazidi kufuata maagizo wanayopewa na wizara ya afya na wachukulie virusi vya Corona kwa makini mno.

Mapema wiki hii, rais Uhuru Kenyatta aliwaamuru mawaziri wote wasitoke nje ya jiji la Nairobi baada ya mawaziri watatu kupatikana na virusi hivyo.

Oguna amekuwa katika mstari wa mbele kupambana na virusi hivyo, huku mara kwa mara akiandamana na waziri wa afya Mutahi Kagwe katika kaunti tofauti.

Ni takribani zaidi ya siku mia moja tangu Kenya kusajili au kurekodi kisa cha kwanza. Kutoka kwetu wanajambo tunamtakia afueni ya haraka.

Kufikia sasa Kenya imerekodi visa 16,268 vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo 274, huku wagonjwa 7,446 wakithibitishwa kupona ugonjwa huo hatari.