TANZANIA-CHADEMA-SIASA-USALAMA

Tundu Lissu arejea nchini Tanzania

Tundu Lissu, ni wakili na mwanasiasa mwenye umri wa miaka 58, lakini pia  Naibu Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini humo  CHADEMA.
Tundu Lissu, ni wakili na mwanasiasa mwenye umri wa miaka 58, lakini pia  Naibu Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini humo  CHADEMA. Tundu Antiphas Lissu/twitter.com

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu ambaye amekuwa akipata matibabu nchini Ubelgiji, baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana jijini Dodoma mwaka 2017, amerejea nchini na kulakiwa na umati wa wafuasi wake katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam.

Matangazo ya kibiashara

Tundu Lissu aliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere majira ya saa nane mchana, saa za Afrika Mashariki, akitokea nchini Ubelgiji ambako amekuwa akipata matibabu zaidi.

 

Tindu Lissu alishangiliwa kwa shangwe na mapokezi yake yalionekana kuwa ya amani ingawa siku ya Jumamosi, polisi nchini Tanzania ilitoa tamko la kupiga marufuku mikusanyiko ya watu siku ya Jumatatu ya Julai 27.

 

Hata hivyo viongozi wa chama cha upinzani cha CHADEMA wamekuwa wakihamasisha wananchi kujitokeza kwenda kumpokea mwanasiasa wa chama hicho Tundu Lissu.

 

Tundu Lissu, ni wakili na mwanasiasa mwenye umri wa miaka 58, lakini pia  Naibu Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini humo  CHADEMA.

Amekuwa mkosoaji mkubwa wa rais John Magufuli, kusababisha kukamatwa kwake mara kadhaa.

Mwaka 2017, alikamatwa na maafisa wa usalama mara sita kwa kile kilichoelezwa ni kumkosea heshima rais Magufuli  kwa  kumwita Dikteta.

Mambo yalikuwa mabaya zaidi mwezi Septemba mwaka 2017 wakati wa kikao cha bunge jijini Dodoma, aliposhambuliwa na watu wasiojuliana na na kujeruhiwa vibaya.

Alipata majereha 18 katika mwili wake na kukimbizwa jijini Nairobi nchini Kenya kupata matibabu kabla ya kuhamishiwa nchini Ubelgiji kupata matibabu zaidi.

Baada ya mkasa huo, rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Twitter, aliandika kusikitishwa na kushambuliwa kwa Lissu, na kumtakia nafuu ya haraka.

Kushambuliwa kwa Lissu, kumeendelea kulaaniwa na watetezi wa haki za binadamu na viongozi wa dini nchini Tanzania, na ameamua kurejea nyumbani licha ya wito wa familia yake kumtaka asifanye hivyo.

Wakili wake ameindikia barua serikali ya Tanzania, kutaka mwanasiasa huyo kupewa ulinzi atakapowasili nchini humo.

Tundu Lissu, amechukua fomu ya kuomba tiketi ya kuwania urais kupitia chama chake cha CHADEMA wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.