KENYA-CORONA-AFYA

Kenya yachukua hatua kuzuia wimbi jipya la Corona

Kenya inaendelea kuripoti visa zaidi vya maambukizi ya viriusi vya Corona.
Kenya inaendelea kuripoti visa zaidi vya maambukizi ya viriusi vya Corona. AFP / LUIS TATO

Wiki tatu baada ya kulegeza baadhi ya masharti dhidi ya janga la Corona, hatimaye Kenya imeimarisha hatua za kukabiliana dhidi ya mlipuko mpya wa visa vya maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo hatari.

Matangazo ya kibiashara

Sheria ya kutotoka nje imesogezwa mbele kwa siku thelathini, mikahawa imetakiwa kufungwa kuanzia saa moja usiku, vilabu vimefungwa kabisa na uuzaji wa pombe umepigwa marufuku kote nchini.

Kufikia sasa Kenya imerekodi visa 18,000 vya maambukizi ya virusi vya Covid-19, idadi ya visa vya maambukizi imeongezeka zaidi kwa kipindi cha wiki tatu nchini Kenya.

Hali inaweza kuwa mbaya zaidi mwezi ujao wa Agosti au Septemba ikiwa hatua kali hazitachukuliwa dhidi ya ugonjwa huo hatari.

Serikali na viongozi wakaunti walikutana Jumatatu hii, Julai 27 ili kujadili jinsi ya kukabiliana na mlipuko huo mpya. Kaunti tano tu kati ya arobaini na saba nchini zitakuwa na uwezo wa kudhibiti idadi kubwa ya wagonjwa katika siku za usoni. Matokeo ambayo yamezua sintofahamu baada ya ugunduzi wa uchunguzi uliofanywa na mamlaka. Angalau magavana wa kaunti ishirini inasemekana walisema uwongo juu ya kiwango cha uwezo wao, hususan kuhusu idadi ya vitanda katika hospitali.

Licha ya hali kuwa mbaya zaidi, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta hajawa tayari kuchukuwa hatua ya kuzuia maambukizi zaidi kususan kupiga marufuku watu kutembea wakati mgogoro wa kiuchumi unaendelea kushika kasi nchini humo kutokana na janga la Corona. Lakini ametoa wito wa kila mmoja kuchukuwa maamuzi ya kukabiliana dhidi ya Covid-19.

Hata hivyo rais Kenyatta alionya kwamba iwapo hali itazorota na kutoa changamnoto kwa sekta ya afya , atarudisha masharti hayo.