TANZANIA-MKAPA-SIASA

Mwili wa Benjamin Mkapa wawasili Lupaso, Kusini mwa Tanzania

Picha ya zamani inaonyesha Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, Desemba 9, 2005, wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 44 ya uhuru wa Tanzania.
Picha ya zamani inaonyesha Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, Desemba 9, 2005, wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 44 ya uhuru wa Tanzania. MWANZO MILLINGA / AFP

Maelfu ya Watanzania wamekusanyika katika uwanja wa Uhuru kumwaga rais wao wa zamani Benjamin Mkapa aliyefariki dunia wiki iliyopita na anayetarajiwa kuzikwa kesho katika kijiji alichozaliwa cha Lupaso katika Wilaya ya Masasi, Kusini mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Rais John Magufuli amewaongoza waombolezaji hao wakiwemo wawakilishi wa maitafa ya kigeni nchini humo, huku Burundi ikiwakilishwa na Waziri Mkuu wake Alain-Guillaume Bunyoni.

Magufuli amemkumbuka mtangulizi wake kama mtu muhimu katika maisha yake, aliyemsaidia kwa mengi na wakati wa hotuba yake, alionekana kutoa machozi.

Tayari mwili wa Mkapa umewasili katika kijiji alichozaliwa kwa mazishi.

Mkapa aliyeongoza Tanzania kati ya mwaka 1995-2005 alifariki dunia kutokana na mshtuko wa moyo.