KENYA-CORONA-AFYA-UCHUKUZI

Viwanja vya ndege vya Kenya vyafunguliwa tena kwa wasafiri kutoka nchi 11

Waziri wa Uchukuzi waKenya,  James Macharia, amesema kuwa anga la Kenya halitafunguliwa kwa kila mtu.
Waziri wa Uchukuzi waKenya, James Macharia, amesema kuwa anga la Kenya halitafunguliwa kwa kila mtu. REUTERS/Baz Ratner

Kenya inatarajiwa kurejelea safari za ndege za Kimataifa hapo kesho licha ya nchi hiyo kuendelea kukabiliwa na ongezeko la maambukizi ya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Waziri wa Uchukuzi nchini humo James Macharia amesema kuwa anga la Kenya halitafunguliwa kwa  nchi zote isipokuwa tu nchi 11 ambazo ni pamoja na China, Korea Kusini, Japan, Canada, Zimbabwe, Ethiopia, Switzerland, Uganda, Rwanda, Namibia na Morocco.

“ Raia wa nchi 11 pekee wa kigeni ndio wanaoruhusiwa kutua Kenya katika viwanja vyake vinne vya kimataifa vilivyopo Nairobi, Mombasa, Eldoret na Kisumu, “ amesema James Macharia.

Hata hivyo, katika orodha ya nchi hiyo, Tanzania ambayo iliacha kutangaza maambukizi ya Corona mwezi Aprili na baadaye rais John Magufuli kusema kuwa nchi hiyo haina tena maambukizi hayo, haimo kwenye orodha hiyo.