UGANDA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Uganda yaendelea kuripoti visa zaidi vya maambukizi

Kampala, mji mkuu wa Uganda.
Kampala, mji mkuu wa Uganda. REUTERS/James Akena/File Photo

Uganda sasa imeripoti kifo cha nne kinachotokana na maamukizi ya virusi vya Corona, wakati huu serikali nchini humo ikiwaonya raia kuacha kupuuza kanuni za Wizara ya afya.

Matangazo ya kibiashara

Wahudumu wa afya 10 na wagonjwa 68 katika hospitali ya Kabale Magharibi mwa Uganda wamewekwa karantini, baada ya baadhi ya wagonjwa kupatikana na virusi vya Corona katika nchi hiyo ambayo ina maambukizi zaidi ya watu Elfu Nane.

Kufikia sasa Uganda ina visa 1,182 vya maambukizi ya virusi vya Corona, na wagonjwa 1,045 wamepona ugonjwa huo hatari.

Hayo yanajiri wakati visa Milioni 18 vya maambukizi vimeripotiwa kote duniani, baada ya visa Laki 2 na Elfu 64 kuthiobitishwa na wagonjwa Milioni 10.7 wamepona ugonjwa wa Covid-19.

Idadi ya vifo imefikia Laki 6 na Elfu 89, baada ya vifo vipya 5,901 kuthibitishwa.

Mwishoni mwa wiki hii iliyopita Shirika la Afya duniani WHO lilionya kuwa janga la virusi vya Corona litadumu kwa muda mrefu na huenda likasababisha ''kuelemewa kwa mikakati ya kukabiliana nalo".