KENYA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya vifo yapindukia 382 Kenya

Kenya inaendelea kuripoti visa zaidi vya maambukizi ya virusi vya Corona.
Kenya inaendelea kuripoti visa zaidi vya maambukizi ya virusi vya Corona. REUTERS/Baz Ratner

Watu wengine 13 wamepoteza maisha nchini Kenya kutokana na virusi vya Corona na kufikisha idadi ya vifo kufikia 382, huku wengine 544 wakiambukizwa na kufikisha idadi ya maambukizi kufikia 22,597. Idadi ya watu waliopona imefikia 8,740.

Matangazo ya kibiashara

Jiji kuu Nairobi limeendelea kushuhudia ongezeko la maambukizi, huku watalaam wa afya wakihusisha ongezeko hilo na msimu wa baridi ambao umekuwa ukishuhudiwa tangu mwezi Julai.

Wakati huo huo walimu wa shule za binafsi nchini Kenya wanalalamikia hali ya maisha ambayo imekuwa ngumu kutokana na janga la corona, wakibaini kwamba ugonjwa wa Covid-19 umewaathiri pakubwa.

Walimu hao, ambao baada ya Shule kufungwa wamelazimika kutafuta kazi ndogo ndogo ili kujikimu kimaisha.

Hivi karibuni serikali ya Kenya ilichukuwa hatua ya kulegeza masharti ya kukabiliana dhidi Corona ikibaini kwamba ilifanya hivyo kwa kunusuru uchumi wa nchi hiyo ambao umedorora kutokana na janga hilo hatari.

Hayo yanajiri wakati shirika la Afya Duniani WHO limeonya kuwa licha ya kuwepo matumaini makubwa ya chanjo ya virusi vya corona, huenda kusiwe na tiba ya haraka ya ugonjwa wa Covid-19 na kwamba itachukua muda mrefu kabla hali irudi kuwa ya kawaida.