UGANDA-TANZANIACORONA-AFYA

Coronavirus: Uganda yachukuwa hatua za kudhibiti maambukizi kwenye mpaka wake na Tanzania

Katika miezi ya hivi karibuni Kenya ilichukuwa hatua ya kufunga mpaka wake na Tanzania kwenye eneo la mpaka la Lunga-Lunga.
Katika miezi ya hivi karibuni Kenya ilichukuwa hatua ya kufunga mpaka wake na Tanzania kwenye eneo la mpaka la Lunga-Lunga. Joseph Jira/RFI

Serikali ya Uganda, imeanza kudhibiti biashara na watu kuingia na kutoka nchini humo kwenye mpaka wake na Tanzania eneo la Mutukula, katika mkakati wa kudhibiti kusambaa zaidi kwa virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Hii inajiri baada ,watu 20 waliokuwa wamewasili nchini kutoka Tanzania hivi majuzi kuthibitishwa kuambukizwa Corona.

Uganda kufikia sasa ina maambuzi 1,213 na vifo vitano vinavyohusishwa na Corona.

Hivi karibuni shirika la Afya Duniani, WHO, liliaonya kuwa licha ya jitihada zinazofanyika kutafuta chanjo na dawa ya kupambana na janga la virusi vya Corona, huenda kusiwe na suluhu ya muda mrefu ya kukabiliana na janga hili.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alionya kuwa hali itaendelea kuwa mbaya zaidi iwapo mataifa mbalimbali duniani hayatachukua hatua zaidi za kukabiliana na virusi hivyo.

Tedros Adhanom Ghebreyesus alitoa wito kwa nchi zote kutilia mkazo hatua muhimu za kiafya ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo ikiwa ni pamoja na kuwalazimisha raia wao kuvaa barakoa, kuwataka raia wasikaribiane kwa mita kadhaa, na kuwataka kuosha mikono kila mara bila kusahau kupima virusi hivyo.

Hata hivyo WHO imeendelea kukosoa hatua zilizochukuliwa hivi karibuni na baadhi ya nchi duniani kwa kulegeza masharti ya kukabiliana na janga la Covid-19, ikisema kuwa Covid-19 bado ni tishio duniani.