KENYA-CORONA-AFYA

Kenya yaendelea kuathirika na maambukizi ya virusi ya Corona

Maafisa wa afya katika manispaa ya jiji la Nairobi wakinyunyuzia dawa dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona katika soko kuu la Nairobi, Kenya, Mei 2, 2020.
Maafisa wa afya katika manispaa ya jiji la Nairobi wakinyunyuzia dawa dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona katika soko kuu la Nairobi, Kenya, Mei 2, 2020. REUTERS/Njeri Mwangi

Wizara ya afya nchini Kenya inasema, watu 48 kutoka famila moja katika Kaunti ya Migori, waliambukizwa virusi vya Corona kutoka kwa mwanafamilia mmoja aliyekuwa amesafiri kutoka jijini Nairobi, huku  nchini hiyo ikiripoti maambukizi mapya 671.

Matangazo ya kibiashara

Watu waliopona kutokana na maambukizi hayo sasa idadi imefikia 9,930, huku wengine 391 wakipoteza maisha tangu kuzuka kwa janga hilo nchini humo.

Katika hatua nyingine, Wiazara ya fedha nchini humo, imeanza kufanya ukaguzi wa matumizi ya Mabilioni ya fedha ya walipa kodi na zile kutoka kwa wafadhili kama Shirika la Fedha duniani IMF, zinavyotumika katika vita dhidi ya virusi vya Corona.

Kufikia sasa ugonjwa wa Covid-19 umesababisha vifo vya watu 706,000 duniani baada ya vifo vipya 5 134 kuthibitishwa, huku visa Milioni 18.8 vya maambukizi vikiripotiwa, baada ya visa vipya laki 2 na Elfu 12 vya maambukizi kuthibitishwa. Wagonjwa Milioni 11.3 wakithibitishwa kupona ugonjwa huo.

Hayo yanajiri wakati China na Shirika la Afya Duniani, WHO, zinajadili mipango ya kubaini chanzo cha mripuko wa virusi vya corona, kufuatia ziara nchini humo, ya wataalamu wawili wa shirika hilo la Umoja wa Mataifa.

Virusi vya Corona vilibainika kwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan katikati mwa China, mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, na vimehusishwa na soko la jumla la vyakula, ambako wanyama wa porini wanauzwa.