TAnzania-MEMBE-ACT-SIASA

Membe apitishwa kupeperusha bendera ya chama cha ACT-Wazalendo

Bernard Membe amesema amejiunga na chama cha ACT-Wazalendo kama mwanachama wa kawaida lakini yuko tayari kutumikia chama hicho kwa ngazi na namna yoyote ile.
Bernard Membe amesema amejiunga na chama cha ACT-Wazalendo kama mwanachama wa kawaida lakini yuko tayari kutumikia chama hicho kwa ngazi na namna yoyote ile. Dotto Rangimoto/twitter.com

Nchini Tanzania, Mshauri Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje Bernard Membe ameidhinishwa kupeperusha bendera ya chama hicho wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba.

Matangazo ya kibiashara

Membe alijiunga na ACT-Wazalendo baada ya kufukuzwa katika chama tawala CCM.

Hata hivyo Membe amesema amejiunga na chama cha ACT-Wazalendo kama mwanachama wa kawaida lakini yuko tayari kutumikia chama hicho kwa ngazi na namna yoyote ile.

Naye Mwenyekiti wa chama hicho Seif Sharif Hamad, ameidhinishwa kuwania urais Visiwani Zanzibar na kutaka Uchaguzi kuwa huru na haki.

Katika hatua nyingine, rais John Magufuli anayetetea kiti hicho kupitia chama tawala CCM, anatarajiwa kupokea fomu za kuwania tena katika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi jijini Dodoma hivi leo.

Uchaguzi wa rais nchini Tanzania unatarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2020.