RWANDA-CORONA-AFYA

Visa vya maambukizi vyapungua siku tatu mfululizo nchini Rwanda

Kwa miezi nne, Rwanda imeendelea kuchukua hatua kali barani Afrika katika kupambana dhidi ya maambukizi ya Corona.
Kwa miezi nne, Rwanda imeendelea kuchukua hatua kali barani Afrika katika kupambana dhidi ya maambukizi ya Corona. SIMON WOHLFAHRT / AFP

Kwa siku ya tatu Rwanda imeripoti idadi ya chini ya maambukizi ya Corona ya watu saba huku idadi ya watu  wengine 21 wakiripotiwa kupona.

Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa Rwanda ina visa  elfu mbili mia moja kumi na moja watu watano wakiripotiwa kufariki dunia kutokana na Corona.

Hayo yanajiri wakati mataifa mengi yameendelea kurekodi idadi kubwa ya maambukizi virusi hivyo wakati Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona barani Afrika imefikia zaidi ya Milioni Moja, huku idadi hiyo ikifikia Milioni 19 duniani. Idadi ya vifo imepindukia 712,000, huku wagonjwa Milioni 11.5 wakithibitishwa kupona duniani kote.

Nusu ya maambukizi hayo yameripotiwa nchini Afrika Kusini, ambayo kwa sasa watu zaidi ya Laki Tano na Elfu 30 wameambukizwa.

Misri, Nigeria na Ghana pia ni mataifa mengine yenye idadi kubwa ya maambukizi, huku idadi ya watu waliopoteza maisha ikifikia 9,604.

Daktari John Nkengasong, Mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika, CDC amesema, bara la Afrika lina nafasi ya kushinda janga hili.

Hata hivyo hivi karibu shirika la Afya Duniani, WHO, lilisema linahofia ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika, huku likionya kuwa kuendelea kushuhudiwa kwa ongezeko hilo hasa nchini Afrika Kusini, huenda hatua hiyo ikaathiri mataifa mengine barani Afrika.