BURUNDI-RWANDA-USHIRIKIANO

Uhusiano kati ya Burundi na Rwanda: Rais wa Burundi afutilia mbali ombi la rais wa Rwanda

Wiki chache zilizopita, Rais wa Rwanda Paul Kgame aliutaka utawala mpya wa Burundi "kufunua ukurasa mpya" baada ya miaka mitano ya mvutano kati ya mataifa hayo mawili jirani.

(Picha ya kumbukumbu) Évariste Ndayishimiye wakati wa kuapishwa kwake kama rais mpya wa Burundi, kwenye uwanja wa soka wa Gitega, Juni 18, 2020.
(Picha ya kumbukumbu) Évariste Ndayishimiye wakati wa kuapishwa kwake kama rais mpya wa Burundi, kwenye uwanja wa soka wa Gitega, Juni 18, 2020. Tchandrou NITANGA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatimaye rais wa Burundi amemjibu hivi punde kwa kupinga ombi hilo kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa twitter wa ikulu ya rais huko Bujumbura.

Jenerali Evariste Ndayishimiye amemjibu mwenzake wa Rwanda kulingana na ujumbe kwenye ukurasa wa twitter wa ikulu ya rais ya Burundi, ambayo jana ilirusha baadhi ya maneno ya hotuba ya rais aliyoitoa siku moja kabla katika wilaya ya Busoni, Kaskazini Mashariki mwa nchi, karibu na mpakani na Rwanda.

Katika hotuba hiyo, Evariste Ndayishimiye anafutilia mbali ombi la Paul Kagame akimtuhumu kuwa "mnafiki". Rais aw Burundi anachukulia barua ya wazi iliyoandikwa na wakimbizi watano wa nchi hiyo walio nchini Rwanda wanaodai kuwakilisha wengine 300, na ambao wanadai kukuwa wametekwa nyara nchini Rwanda.

"Tunataka kuwa na uhusiano mzuri na nchi zote jirani au nchi za mbali ambazo ziliwapa hifadhi wakimbizi wa Burundi. Lakini hatutakuwa na uhusiano mzuri na nchi ambayo hutumia mafisadi, nchi ya kinafiki, ambayo inadai kutaka kufufua uhusiano mzuri na Burundi wakati huo huo inatutega ili tuweze tuweze kujibamiza.

Lakini tunajua ni kwanini waliteka nyara wakimbizi wa Burundi. Walifanya hivyo kuwafanya kama ngao kwa uhalifu uliogharimu maisha ya watu wengi nchini Burundi mwaka 2015.

Ikiwa wanataka kabisa kuwa na uhusiano mzuri na Burundi, watukabidhi wahalifu waishio nchini humo ili tuweze kuwahukumu, kwa sababu Warundi hawatapata amani kwa muda mrefu kama wale waliohusika na mzozo wa mwaka 2015 [maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza na ukandamizaji walioufanya] hawataadhibiwa.

"Maneno ya Evariste Ndayishimiye yalikusanywa na kutafsiriwa na Esdras Ndikumana, kutoka kitengo cha RFI kanda ya Afrika (RFI-Afrique).