UGANDA-CORONA-AFYA

Uganda yakabiliwa na ongezeko la maambukizi ya Corona

Msafiri huyu akivaa barakoa kama njia ya kuzuia dhidi ya kuenea kwa maambukizi ya COVID-19, wakati akisubiri basi ya mjini kati katika kituo cha mabasi cha Namirembe huko Kampala, Uganda Juni 4, 2020, siku ya kwanza ya kufunguliwa kwa usafiri wa umma.
Msafiri huyu akivaa barakoa kama njia ya kuzuia dhidi ya kuenea kwa maambukizi ya COVID-19, wakati akisubiri basi ya mjini kati katika kituo cha mabasi cha Namirembe huko Kampala, Uganda Juni 4, 2020, siku ya kwanza ya kufunguliwa kwa usafiri wa umma. Badru KATUMBA / AFP

Wizara ya afya nchini Uganda imethibitisha kuwa, mgonjwa mwingine wa virusi vya corona amefariki dunia, na kufikisha idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na janga hili kufikia saba katika nchi hiyo ambayo ina maambukizi zaidi ya Elfu Moja na Mia Mbili.

Matangazo ya kibiashara

Uganda ilitangaza kifo chake cha kwanza kinachohusiana na Covid-19 hivi karibuni, Julai 23. Tangu wakati huo, ugonjwa huo unaonekana kuendelea kushiika kasi nchini humo.

Ubalozi wa Marekani nchini humo nao umedai kuwa, kuna maambukizi makubwa jijini Kampala, tofauti na yale yanayoripotiwa na serikali nchini humo.

Halmashauri ya manispaa ya jiji la Kampala imeanza kusambaza barakoa katika vitongoji vya jiji hilo. Mamlaka pia imeongeza kampeni za kuwahimioza wananchi kupambana dhidi ya Corona.

Mwishoni mwa mwezi Julai rais Museveni alitangaza kulegeza sehemu ya hatua zilizochukuliwa nchini kwa kudhibiti janga hilo, haswa kurejesha hali ya kawaida kwa kufnguwa tena baadhi ya biashara, kulegeza sheria ya kutotoka nje na kuwaruhusu waendesha pikipiki za kukudiwa kufanya tena shughuli yao.

Mbali na hilo, kuelekea Uchaguzi Mkuu mapema mwaka ujao, wanasiasa wa upinzani wanalalamikia kuonewa  na polisi wakati wanapokusanyika kwa kuzingatia kanuni za Wizara ya afya, kinyume na wale wa chama tawala NRM.