Marufuku kurusha matangazo ya kimataifa bila ya kibali Tanzania
Imechapishwa:
Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya mawasiliano nchini humo TCRA, marufuku kwa Redio na Televisheni kurusha maudhui kutoka kwenye vyombo vya habari vya Kimataifa bila ya kuwa na leseni.
Tangazo lililotolewa na mamlaka hiyo linasema kwamba kanuni hizo mpya zimeanza kutumika tangu Julai mosi mwaka 2020, na kwamba radio na televisheni nchini zinazoendelea kurusha matangazo ya kimataifa zitakuwa zinaeendelea kutenda makosa kurusha matangazo hayo bila Kigali.
Hii imekuja baada ya serikali nchini humo, kufanyia marekebisho Kanuni zake za Maudhui ya Redio na Televisheni, mabadiliko ambayo yamezua maswali kuhusu uhuru wa vyombo vya Habari nchini humo.
Kanuni hizo hazijasema lolote kama maombi hayo yatachukuwa muda gani kujibiwa mbali ya kusisitiza kwamba mkurugenzi mkuu wa tcra ana mamlaka ya mwisho kuhusu kuwepo kwa mashikiano hayo.
Mabadiliko haya yamepokelea kwa hisia tofauti na waandishi wa habari pamoja na wakuu wa vyombo vya habari,ambapo baadhi yao wameitaka mamlaka hiyo kuangalia upya uamuzi wao.