KENYA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya vifo yapindukia 438 nchini Kenya

Kenya inaendelea kuripoti visa zaidi vya maambukizi ya virusi vya Corona.
Kenya inaendelea kuripoti visa zaidi vya maambukizi ya virusi vya Corona. REUTERS/Thomas Mukoya

Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Kenya kutokana na janga la Corona, imefikia 438 baada ya watu wengine 15 kufariki duniani kwa muda wa saa 24 zilizopita.

Matangazo ya kibiashara

Aidha, idadi ya watu walioambukizwa imeongezeka na kufikia zaidi ya watu Elfu 27 na 400 baada ya watu wengine 497 kuripotiwa kuambukizwa.

Waziri wa Afya nchini humo Mutahi Kagwe ameendelea kuwataka raia wa nchi hiyo kuendelea kuchukua tahadhari kuzuia maambukizi haya.

Wakati nchi hiyo ikiendelea kukabiliana na janga hilo, Wizara ya afya imeendelea kupata shinikizo za kuweka wazi kuhusu namna inavyotumia fedha za kukabiliana na janga hilo.

Virusi vya Corona vilibainika kwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan katikati mwa China, mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, na vimehusishwa na soko la jumla la vyakula, ambako wanyama wa porini wanauzwa.

Hivi karibuni shirika la Afya Duniani, WHO, lilionya kuwa licha ya jitihada zinazofanyika kutafuta chanjo na dawa ya kupambana na janga la virusi vya Corona, huenda kusiwe na suluhu ya muda mrefu ya kukabiliana na janga hili.