SUDANI KUSINI-USALAMA

Zaidi ya themanini waangamia katika makabiliano ya risasi Warrap, Sudan Kusini

Askari wa jeshi la Sudan Kusini (SSPDF), ambalo zamani liliitwa jeshi la ukombozi wa raia Sudan Kusini (SPLA).
Askari wa jeshi la Sudan Kusini (SSPDF), ambalo zamani liliitwa jeshi la ukombozi wa raia Sudan Kusini (SPLA). Alex McBride / AFP

Watu zaidi ya Themanini, wameuawa katika jimbo la Warrap nchini Sudan Kusini, baada ya kushuhudiwa kwa mapigano makali kati ya wanajeshi na raia wanaomiliki silaha.

Matangazo ya kibiashara

Mauaji haya yamethibitishwa na serikali jijini Juba na Umoja wa Mataifa, ambao umesema hali hii imetokea wakati jeshi lilipokuwa linawapokonya silaha raia wanaozimiliki kwa nguvu.

Ripoti zinasema, wanajeshi zaidi ya Hamsini wameuawa katika makabiliano hayo makali, ambayo yamekuwa yakishuhudiwa tangu mwishoni mwa wiki iliyopita.

Licha ya kuundwa kwa serikali ya pamoja, nchi ya Sudan Kusini imeendelea kushuhudia utovu wa usalama tangu mwaka 2013.