KENYA-CORONA-AFYA

Corona: Idadi ya maambukizi yazidi 30,000 nchini Kenya

Mabango yaliyowekwa sehemu mbalimbali nchini Kenya yanayohimiza raia kuosha mikono na kuvaabarakoa kama hatua za kinga dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, katika eneo la Kibera jijini Nairobi, Agosti 13, 2020.
Mabango yaliyowekwa sehemu mbalimbali nchini Kenya yanayohimiza raia kuosha mikono na kuvaabarakoa kama hatua za kinga dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, katika eneo la Kibera jijini Nairobi, Agosti 13, 2020. Simon MAINA / AFP

Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Kenya, sasa imevuka elfu 30 baada ya watu wengine 271 kuthibitishwa kuambukizwa. Kenya imeendelea kuripoti visa vingi vya maambukizikatika siku za hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe kwenye taarifa kwa vyombo vya habari amesema idadi ya watu waliopona wamefikia elfu 16 mia sita hamsini na sita baada ya watu wengine 686 kupona ugonjwa huo.

Hayo yanajiri wakati dunia sasa ina maambukizi Milioni 21.6M baada ya wagonjwa wapya laki 2 na elfu 68 kuthibitishwa, huku vifo laki 7 na elfu 74 vikithibitishwa baada ya vifo vipya 5,993 kuripotiwa. Hata hivyo wagonjwa Milioni 13.6 wamepona ugonjwa huo hatari.

Hivi karibuni shirika la Afya Dunia, WHO lilizitaka nchi zote kutilia mkazo hatua za kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.

Shirika hilo liliaonya kuwa licha ya jitihada zinazofanyika kutafuta chanjo na dawa ya kupambana na janga la virusi vya Corona, huenda kusiwe na suluhu ya muda mrefu ya kukabiliana na janga hili.

WHO imeendelea kukosoa hatua zilizochukuliwa hivi karibuni na baadhi ya nchi duniani kwa kulegeza masharti ya kukabiliana na janga la Covid-19, ikisema kuwa Covid-19 bado ni tishio duniani.