BURUND-UJERU%ANI-UBELGIJI-USHIRIKIANO

Burundi kudai Ubelgiji na Ujerumani euro bilioni 36 kama fidia za ukoloni wao

Rais mpya wa Burundi Evariste Ndayishimiye, akiambatana na mkewe Angelique Ndayubaha, katika moja ya vituo vya kupigia kura wilayani Giheta, mkoani Gitega, katikati mwa Burundi, wakati wa uchaguzi wa urais, Mei 20, 2020.
Rais mpya wa Burundi Evariste Ndayishimiye, akiambatana na mkewe Angelique Ndayubaha, katika moja ya vituo vya kupigia kura wilayani Giheta, mkoani Gitega, katikati mwa Burundi, wakati wa uchaguzi wa urais, Mei 20, 2020. AFP

Burundi huenda ikaomba fidia kutoka kwa mataifa ya Ubelgiji na Ujerumani kutokana na madhara yaliyotokea wakati wa ukoloni , kwa mujibu wa ripoti inayoandaliwa na watalaam walioteuliwa na Bunge la Senati.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti za vyombo vya habari zibaini kwamba Burundi inazitaka Ujerumani na Ubelgiji ziilipe euro bilioni 36 kama fidia za ukoloni wao.

Katika enzi za ukoloni, inadaiwa kuwa Ujerumani na Ubelgiji zilichochea mgawanyiko kati ya Wahutu na Watutsi.

Hali hii ilichangia kuzuka kwa mapigano mabaya baina ya makabila hayo mawili katika miaka ya 1970 na mapigano mengine ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa miaka 12 tangu mwaka 1993. Karibu watu laki tatu walipoteza maisha katika mapigano hayo na wengine wengi kuyatoroka makazi yao.

Mwaka 2009, Ubelgiji iliomba msamaha rasmi kwa vitendo hivyo.

Burundi ilikuwa koloni la Ujerumani kutoka 1890 na baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia nchi hiyo ikawa koloni la Ubelgiji mpaka ilipopata uhuru 1962.

Mara tu kiasi cha fidia kitakapoamuliwa, Burundi inapanga kupeleka mapendekezo hayo kwa serikali za Ujerumani na Ubelgiji.