KENYA-SIASA-MAENDELEO

Kenya: Bunge la Seneti lakumbwa na sintofahamu kuhusiana na ugavi wa fedha za maendeleo ya kaunti

Makao makuu ya bunge la Kenya, Nairobi, Mei 2, 2018.
Makao makuu ya bunge la Kenya, Nairobi, Mei 2, 2018. REUTERS/Thomas Mukoya

Bunge la Senate nchini Kenya, limeunda Kamati ya Maseneta 12 kukwamua sintofahamu ya kutoelewana kuhusu namna ya kugawana fedha kwenda kwenye Kaunti zote 47.

Matangazo ya kibiashara

Hii imekuja baada ya vikao 10 vya Maseneta hao kushindwa kupata mwafaka suala hili muhimu kwa ajili ya maendeleo ya Kaunti.

Hata hivyo jana, majibizano makali kati ya baadhi ya Maseneta kutoka chama cha tawala na upinzani yalizuka siku nzima, baada ya Maseneta watatu kukamatwa kwa kile kinachoonekana ulikuwa ni mpango wa kuwazuia kupigia kura mapendekezo yao, yanayopingwa na upande wa serikali.

Raia wengi waliokuwa na hasira walimiminika mitaani wakiomba maseneta hao waachiliwe huru. Duru za kuaminika zinabaini kwamba maseneta hao waliachiliwa huru.

Serikali ya Kenya haijasema kuhusiana na kukamatwa kwa maseneta hao.