KENYA-CORONA-AFYA

Kenya yakanusha kutumia vibaya fedha za wahisani katika kukabiliana na janga la Corona

kenya imerekodi visa vingine 271 vya maambukizi ya Corona na kufanya idadi ya maambukizi kufikia Elfu 30 na 636.
kenya imerekodi visa vingine 271 vya maambukizi ya Corona na kufanya idadi ya maambukizi kufikia Elfu 30 na 636. REUTERS/Jackson Njehia

Wizara ya afya nchini Kenya imekanusha ripoti za ubadhirifu mkubwa wa fedha za wahisani zilizotolewa kukabiliana na janga la Corona, linaloendelea kuiathiri nchi hiyo ya Afrika ya Mashariki.

Matangazo ya kibiashara

Kituo cha Televisheni cha NTV kilitoa ripoti ya uchunguzi iliyoonesha kuwa zaidi ya Dola za Marekani Milioni 400 hazijulikani zilivyotumika.

Hayo yanajiri wakati huu, nchi hiyo ikiripoti visa vingine 271 vya maambukizi ya Corona na kufanya idadi ya maambukizi kufikia Elfu 30 na 636.

Kenya imeendelea kurekodi visa zaidi vya maambukizi, huku idadi ya vifo ikifikia 487 wakati wagonjwa 17,368 wakithibitishwa kupona.

Hivi karibuni shirika la Afya Duniani, WHO lilisema bara la Afrika litaendelea kushuhudia ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona wakati huu nchi nyingi zinapoanza kufungua mipaka yake na maisha kuanza kurejea taratibu, katika bara hilo ambalo lina maambukizi zaidi ya Milioni Moja.

WHO pia lilisema linahofia ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika, huku likionya kuwa kuendelea kushuhudiwa kwa ongezeko hilo hasa nchini Afrika Kusini, huenda hatua hiyo ikaathiri mataifa mengine barani Afrika.