KENYA-MGOMO-CORONA-AFYA

Sekta ya afya kukabiliwa na mgomo Kenya

Kenya imeripoti visa vingine 426 na kufanya idadi ya maambukizi siku ya Alhamisi kufikia 31,441, huku watu wengine 10 wakipoteza maisha.
Kenya imeripoti visa vingine 426 na kufanya idadi ya maambukizi siku ya Alhamisi kufikia 31,441, huku watu wengine 10 wakipoteza maisha. TONY KARUMBA / AFP

Wahudumu wa afya nchini Kenya watishia kugoma baada ya wiki tatu zijazo, iwapo serikali haitatekeleza matakwa yao ya kutaka usalama katika maeneo ya kazi, wakati  huu nchi hiyo inapoendelea kukabiliwa na janga la Corona.

Matangazo ya kibiashara

Tangu mwezi Mei, mazungumzo kati ya chama cha wahudumu hao wa afya na Wizara ya Kazi, yamekuwa yakiendelea lakini hakuna mwafaka wowote uliopatikana.

Hii inakuja wakati huu nchi hiyo ikiripoti visa vingine 426 na kuanya idadi ya maambukizi siku ya Alhamisi kufikia 31,441, huku watu wengine 10 wakipoteza maisha.

Kwa upande mwingine kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika CDC, kinasema kuwa idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona barani humo imeanza kushuka kuanzia wiki iliyopita. Hii ikitafsiriwa kuwa ishara nzuri ya bara hili kufanikiwa katika mapambano dhidi ya janga hili.

Mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti magonjwa barani Dkt John Nkengasong amesema  ingawaje ugonjwa huo ulikuwa hatari ,kuna matumaini ya kuushinda.

Afrika kufikia sasa ina zaidi ya maambukizi milioni moja ,Afrika Kusini ikichangia kiasi kikubwa.