KENYA-CORONA-AFYA-UFISADI

Kenya: Mapambano dhidi ya Covid-19 yakumbwa na kashfa ya ufisadi

Nairobi, mji mkuu wa Kenya.
Nairobi, mji mkuu wa Kenya. Sam Stearman/Wikipédia

Katika mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Covid-19 nchini Kenya, kunaripotiwa matumizi mabaya ya mamilioni ya Dola na vifaa vya matibabu na kufikia sasa uchunguzi unaendelea.

Matangazo ya kibiashara

Maandamano kadhaa yalifanyika kupinga ufisadi nchini humo na shinikizo limeongezeka kwa rais Kenyatta, wakati mashirika 25 yasiyo kuwa ya kiserikali, mashirika mbalimbali na vyama vya wafanyakazi vilisainiwa, Jumatatu hii, Agosti 24, taarifa ya pamoja inayomuomba rais Kenyatta kuchukuwa 'hatua'.

 

Maandamano hayo pia yalishuhudiwa katika mji wa Kisumu, magharibi mwa Kenya, jana Jumatatu, kupinga kuendelea kwa ufisadi huo, hasa pale inapokuwa inahusu fedha na vifaa vilivyokusudiwa kutumika katika mapambano dhidi ya Covid-19.

Waandamanaji wamemshtumu rais wa nchi hiyo kuendelea kukaa kimya na hivyo kuchukuliwa kuwa anaunga mkono wahalifu hao.

Kwa upande wa mamlaka ya vifaa vya matibabu ambapo ufisadi mkubwa umeripotiwa, viongozi wakuu kadhaa wamesimamishwa kazi kwa uchunguzi, lakini mashirika haya 25 yanataka uchunguzi zaidi.Yanahitaji ripoti kamili juu ya idadi ya kitanda, vifaa vilivyopo, wafanyakazi waliotumwa katika hospitali na sehemu mbalimbali kwa minajili ya kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo, lakini pia kuhusu orodha ya kampuni ambayo yalitia saini kwenye mikataba katika muktadha wa mapambano dhidi ya janga hilo.

Washirika wa kimataifa wametakiwa kuelezea mikataba ya misaada iliyosainiwa kati yao na Kenya, taarifa hiyo imebaini.