TANZANIA-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Uchaguzi wa urais Tanzania: John Magufuli kukabiliana na upinzani uliogawanyika

Rais wa Tanzania John Magufuli anakabiliwa na upinzani katika uchaguzi wa urais wa mwezi Oktoba. (picha kumbukumbu)
Rais wa Tanzania John Magufuli anakabiliwa na upinzani katika uchaguzi wa urais wa mwezi Oktoba. (picha kumbukumbu) REUTERS/Thomas Mukoya/File Photo

Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania, NEC (National Electoral Commission) imekubali fomu ya rais wa Tanzania John Pombe Maguli kuwania katika uchaguzi wa urais ujao.

Matangazo ya kibiashara

Magufuli anaye maliza muda wake, ambaye alipewa ridhaa na chama chake cha CCM kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa urais, anatarajia kupambana na wagombea 14 kutoka vyama vikuu vya upinzani.

Hata hivyo upinzani nchini Tanzania umegawanyika, ikisalia tu miezi micache kabla ya uchaguzi wa urais ambao tayari rais Magufuli amepewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama viwili ambavyo kimerithi, vinatawala siasa ya Tanzania tangu nchi hiyo kupata uhuru wake mwaka 1961.

Joto la uchaguzi nchini Tanzania linazidi kupanda ambapo taifa hilo la Afrika Mashariki linafanya uchaguzi wake wa tano tangu kuasisiwa kwa demokrasia ya vyama vingi zaidi ya miongo miwili iliyopita.

Kama ilivyokuwa mwaka 2015, mpinzani mkuu wa rais Magufuli atakuwa mgombea wa chama cha upinzani cha Chadema, ambapo mwaka atakuwa ni Tundu Lissu. Amerejea nchini akitokea uhamishoni kwanza nchini Kenya na kisha Ubelgiji. Miaka mitatu iliyopita, watu wenye silaha walipiga risasi, na kumjeruhi vibaya. Hata hivyo ameendelea kusema kuwa ilikuwa ni jaribio la mauaji ya kisiasa.

Waziri wa zamani wa mambo ya nje pia ni miongoni mwa wagombea 14 wa upinzani watakaopambana dhidi ya Rais Magufu Oktoba 28. Lakini wapinzani, watetezi wa haki za binadamu na waandishi wa habari tayari wana wasiwasi juu ya ukweli wa uchaguzi huo.