RWANDA-HAKI

Rwanda: Paul Rusesabagina, mmiliki wa zamani wa hoteli Mille Collines, akamatwa Kigali

Paul Rusesabagina, wakati aliposhiriki kwenye maandamano yaliyoitwa "tuiokoe Darfur: maandamano kwa minajili ya kusitisha mauaji ya halaiki", Aprili 30, 2006, huko Washington.
Paul Rusesabagina, wakati aliposhiriki kwenye maandamano yaliyoitwa "tuiokoe Darfur: maandamano kwa minajili ya kusitisha mauaji ya halaiki", Aprili 30, 2006, huko Washington. Nancy Ostertag / Getty Images North America / AFP

Paul Rusesabagina anatuhumiwa kuwa mmoja wa waanzilishi na wafadhili wa kundi la waasi wa Rwanda la FDLR na hivi leo anajikuta akishutumiwa ugaidi, utekaji nyara na mauaji.

Matangazo ya kibiashara

Mazingira ya kukamatwa kwake hayajulikani, lakini polisi ya Rwanda inadai kuwa alikamatwa kutokana na "ushirikiano wa kimataifa". Habari hiyo imethibitishwa na idara ya Upelelezi ya Rwanda (Rwanda Investigation Bureau) kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Wakati wa mauaji ya kimbari, Paul Rusesabagina aliwaokoa mamia ya watu wengi kutoka jamii za Watutsi na Wahutu kwenye hoteli yake, kitendo ambacho kilipuuzwa na kutoingizwa katika filamu iliyoitwa Hôtel Rwanda.

Kwa zaidi ya miaka 10, Paul Rusesabagina alikuwa mpinzani wa utawala wa Kigali na aliishi kati ya Ubelgiji na Marekani. Tangu muhula wa 3 wa Paul Kagame, chama chake kiliamini kuwa njia ya mtuto wa bunduki ndio itawezesha kupindua utawala wa rais wa sasa Paul Kagame.