KENYA-CORONA-AFYA

Kenya: Makamu wa rais akabiliwa na kashfa ya ufisadi wa Covid-19

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kushoto) na Makamu wa rais Williame Ruto.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kushoto) na Makamu wa rais Williame Ruto. Yasuyoshi CHIBA / AFP

Wanasiasa na wafanyabiashara wameanza kusikilizwa kufuatia uchunguzi wa madai ya matumizi mabaya ya pesa zilitengwa kwa minajili ya kupambana na virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi kadhaa walisikilizwa wiki hii mbele ya Bunge. Vifaa muhimu vya matibabu vyenye thamani ya dola milioni 400 viliripotiwa kuibiwa.

Makamu wa rais William Ruto pia anaweza kusikiliwa katika kesi hii. kama wanavyodai wanasiasa wengi nchini Kenya.

Kiongozi wa chama tawala, David Murathe, alisikika kwenye mahojiano na vyombo vya habari vya Kenya akitoa wito kwa Tume ya Maadili na Kupambana na Rushwa kumsikiliza Makamu wa rais wa Kenya mwenyewe, William Ruto.

David Murathe alisema William Ruto inashukiwa kuwa ana uhusiano wa karibu na kampuni iliyotajwa katikati ya uchunguzi wa matumizi mabaya ya pesa zilizotengwa kwa minajili ya kupambana na virusi vya Corona.

William Ruto sio kesi yake ya kwanza ya ufisadi. Anaechukuliwa na Wakenya wengi, kuwa mmoja wa wanasiasa wafisadi zaidi nchini, kulingana na uchunguzi.

Kwa wiki kadhaa, kesi hiyo iliibua hisia tofauti miongoni mwa raia. Maandamano yalifanyika katika miji mikubwa na madaktari katika hospitali za umma wanagoma, wameghadhabishwa kwani vituo vingi vinakabiliwa na ukosefu wa vifaa vya matibabu ili kukabiliana na wingi wa wagonjwa.

Uchunguzi ulioagizwa na rais Uhuru Kenyatta unazingatia kuhusu KEMSA, kampuni inayotoa vifaa vya matibabu katika hospitali mbalimbali za serikali.

Dola milioni 400 za vifaa vya matibabu zilipotea pamoja na sehemu ya msaada uliotolewa na bilionea wa China Jack Ma, mwanzilishi wa kapuni ya Alibaba.