RWANDA-SIASA

Rais wa Rwanda akanusha madai ya kutekwa Paul Rusesabagina

Paul Rusesabagina amekuwa akihusishwa kushirikiana na kundi la FNL ambalo mwaka 2018 lilishambulia Kusini mwa nchi hiyo karibu na nchi jirani ya Burundi.
Paul Rusesabagina amekuwa akihusishwa kushirikiana na kundi la FNL ambalo mwaka 2018 lilishambulia Kusini mwa nchi hiyo karibu na nchi jirani ya Burundi. NICOLAS MAETERLINCK / BELGA / AFP

Rais wa Rwanda Paul Kagame, amekanusha kuwa serikali yake ilimteka mpinzani wake Paul Rusesabagina, jijini Dubai na kumrudisha nyumbani ili kufunguliwa mashtaka ya ugaidi na mauaji.

Matangazo ya kibiashara

Rusesabagina anafahamika sana kutokana na filamu ya Hotel Rwanda inayoelezea alivyookoa maisha ya watutsi waliokuwa wamekimbilia katika hoteli moja jijini Kigali wakati wa mauji ya Kimbari mwaka 1994.

Kagame amesema Rusesabagina huenda alidandanywa na kuja nchini Rwanda, hatua iliyopelekea kukamatwa kwake na hakutekwa kama Familia yake inavyodai.

Rusesabagina amekuwa akihusishwa kushirikiana na kundi la FNL ambalo mwaka 2018 lilishambulia Kusini mwa nchi hiyo karibu na nchi jirani ya Burundi.