KENYA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Wauguzi Kenya walalamikia mazingira yao ya kazi na kutishia kufanya mgomo

Madaktari wakiandamana jijini Nairobi, Kenya, Februari 13, 2017.
Madaktari wakiandamana jijini Nairobi, Kenya, Februari 13, 2017. REUTERS/Thomas Mukoya

Madaktari nchini Kenya wametangaza kuanza mgomo baada ya wiki mbili zijazo iwapo hawataongezwa mshahara, na vitendea kazi vyao kutoimarishwa hasa katika kipindi hiki ambacho nchi hiyo inapoendelea kukabiliwa na janga la Corona.

Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa chama cha Madktari nchini humo Chibanzi Mwachonda, amesema wamechoka na ahadi za serikali ambazo amesema hazitekelezwi licha ya mkataba wa kuongezewa mshahara kutiwa saini mwaka 2017.

Tishio hili la Madktari linakuja wakati huu Kenya ikishuhudia kushuka kwa maambukizi ya virusi vya Corona katika siku za hivi karibuni.

Sio mara ya kwanza sekta ya afya nchini Kenya inakumbwa na mgomo kama huo. Wauguzi wanaofanya kazi katika wodi iliyotengwa kwa watu walioambukizwa virusi vya corona nchini Kenya walifanya mgomo baridi mapema mwaka huu kulalamikia kile wanachodai kuwa ukosefu wa vifaa vya kujikinga na mafunzo ya kutosha.