RWANDA-RUSESABAGINA-HAKI

Paul Rusesabagina afunguliwa mashtaka ya ugaidi

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Rusesabagina, aliyekuwa amevamlia barakoa na kuonekana mtulivu, hakuongea Mahakamani ila alioeneka tu akiongea na Mawakili wake.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Rusesabagina, aliyekuwa amevamlia barakoa na kuonekana mtulivu, hakuongea Mahakamani ila alioeneka tu akiongea na Mawakili wake. AFP/Stringer

Paul Rusesabagina, raia wa Rwanda anayekumbukwa kwa kuwaokoa zaidi ya Wanyarwanda zaidi ya Elfu Moja katika hoteli moja jijini Kigali, amefikishwa Mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi.

Matangazo ya kibiashara

Rusesabagina ambaye alikamatwa mwezi uliopita baada ya kurejea jijini Kigali akitokea katika nchi ya Falme za Kiarabu, alifikishwa Mahakamani chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa usalama, huku akiwa na mawakili wake.

Jaji alimsoma mashtaka 12 dhidi ya Rusesabagina ikiwa ni pamoja na ugaidi, mauaji na kuanzisha na kufadhili kundi la kigaidi nchini Rwanda.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Rusesabagina, aliyekuwa amevalia barakoa na kuonekana mtulivu, hakuongea mahakamani ila alioeneka tu akiongea na mawakili wake.

Wakili wake David Rugaza, aliiambia mahakama kuwa mashtaka dhidi ya mteja wake si ya kweli na hastahili kufunguliwa mashtaka hayo na hivyo anastahili kuachiliwa huru.

Rusesabagina ni kiongozi chama cha MRCD ambacho kinashtumiwa kushirikiana na kundi la FLN.