BURUNDI-UN-SIASA-USALAMA

Burundi yataka kurejesha uhusiano wake na Umoja wa Mataifa

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye yuko tayari kufanya kurejesha uhusiano na Umoja wa Mataifa.
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye yuko tayari kufanya kurejesha uhusiano na Umoja wa Mataifa. AFP Photos/Tchandrou Nitanga

Tangu mwaka 2015 kufuatia mgogoro wa kisiasa uliyotokana na uamuzi wa rais wa zamani Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu, uhusiano kati ya Burundi na Umoja wa Mataifa umekuwa mbaya zaidi.

Matangazo ya kibiashara

Pamoja na kuingia madarakani kwa Jenerali Evariste Ndayishimiye miezi miwili iliyopita, hali inaonekana kubadilika.

Serikali ya Burundi sasa inabaini kwamba ukurasa wa mwaka 2015 umefunikwa tangu Jenerali Evariste Ndayishimiye aingie madarakani. Serikali ya Gitega inaitaka Umoja wa Mataifa kuiondoa Burundi katika ajenda ya kisiasa ya Baraza la Usalama. Serikali ya Burundi inataka ushirikiano utakaojikita hasa katika sekta ya kijamii na kiuchumi, kulingana na "Mpango wa Maendeleo wa Kitaifa".

Wakati huo huo jumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa umetumwa nchini Burundi kutathmini hali halisi ya mambo katika nyanja za kijamii na kiuchumi, kisiasa, kibinadamu na haki za binadamu tangu mwaka 2015. Ujumbe huo utakutana wakati wa ziara hiyo na rais Ndayishimiye mara mbili, wajumbe wa serikali, chama tawala na upinzani, viongozi wa dini, vyama vya kiraia na mabalozi mbalimbali wa nchi za kigeni nchini Burundi.

Kwa upande wake, Umoja wa Mataifa pia unataka unataka kuchukuwa hatua dhidi ya utawala ambao unadaiwa kuvunja haki za msingi. Ujumbe huu unaongozwa hasa na Naibu Katibu Mkuu anayehusika na kanda ya Afrika, Bintou Kéita, mmoja wa maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa anayetazamwa kwa jicho zuri na serikali ya Gitega.

Bintou Kéita anapanga pia kuzuru nchi jirani, Uganda, Tanzania, Kenya na Afrika Kusini, pamoja na Addis Ababa, kwa mazungumzo na Umoja wa Afrika.

Ana hadi Oktoba 31 kuwasilisha kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres "ripoti yake ya changamoto zinazoikabili Burundi" na mchango wa umoja huo kwa kukabiliana nazo. Antonio Guterres atakabidhi baadaye nakala yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo kwa sasa limegawanyika kuhusu suala la Burundi, ambalo litachukuwa uamuzi.