TANZANIA-KENYA-USHIRIKIANO

Tanzania na Kenya wamaliza tofauti zao

Kufunguliwa kwa angaa za nchi hizo mbilii, ni ahueni kwa wafanyabishara na watalii ambao sasa watasafiri kwa urahisi kati ya Kenya na Tanzania.
Kufunguliwa kwa angaa za nchi hizo mbilii, ni ahueni kwa wafanyabishara na watalii ambao sasa watasafiri kwa urahisi kati ya Kenya na Tanzania. Wikipédia/Adrian Pingstone

Nchi za Kenya na Tanzania, zimemaliza mvutano wa miezi miwili wa safari ndege kati ya mataifa hayo jirani, uliotokana na namna ya kukabiliana na  janga la virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja, baada ya Kenya siku ya Jumanne kuiondoa Tanzania katika orodha za nchi ambazo raia wake walitakiwa kukaa karantini kwa muda wa siku 14 wanapowasili nchini humo.

Baada ya hatua hiyo ya Kenya, Tanzania kupitia mamlaka ya safari za ndege nayo siku ya Jumatano, ilitangaza kuondoa marufuku iliyokuwa imewekea Mashirika matatu ya ndege ya Kenya kuingia nchini humo.

Shirika la ndege nchini Kenya KQ, limesema litaanza safari zake jiini Dar es salaam siku ya Jumatatu wiki ijayo, huku safari za kwenda Zanzibar zikitarajiwa kuanza tarehe 26, na zitakuwa mara tatu kwa wiki.

Kenya na Tanzania zimetofautiana kuhusu namna ya kukabiliana na janga la Corona.

Tanzania iliacha kutangaza visa vya mamabukizi hayo mwisho wa mwezi Aprili, lakini Kenya imekuwa ikiendelea kutoa takwimu hizo kila siku, na hata kufunga nchi hiyo katika miezi iliyopita.

Kufunguliwa kwa angaa za nchi hizo mbili, ni ahueni kwa wafanyabishara na watalii ambao sasa watasafiri kwa urahisi kati ya Kenya na Tanzania.