RWANDA-KIZITO-TUZO-USANII

Msanii wa Rwanda Kizito Mihigo ashinda tuzo ya kimataifa ya Vaclav Havel

Msanii wa Rwanda Kizito Mihigo Aprili 4, 2019 nyumbani kwake Kigali
Msanii wa Rwanda Kizito Mihigo Aprili 4, 2019 nyumbani kwake Kigali Pierre René-Worms/RFI

Mwanamuziki wa Rwanda Kizito Mihigo aliyefariki dunia mwezi Februari mwaka huu, ni mmoja wa washindi watatu mwaka huu wa Tuzo ya Vaclav Havel. Tuzo hii inapewa kila mwaka wasanii wanaopinga udikteta kwa kazi zao.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa ya Wakfu wa Haki za Binadamu (Human Right Foundation), kwanza amepewa tuzo hiyo kwa kazi ya shirika lake la Mihigo Foundation for Peace kwa kuboresha maridhiano nchini Rwanda.

Kizito Mihigo mwenyewe alikuwa manusura wa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994, na alihubiri amani na maridhiano hasa mashuleni, lakini pia katika magereza, akiwalenga wale ambao walihukumiwa kwa mauaji ya kimbari.

'Ujasiri mkubwa'

Lakini ikiwa amepewa tuzo hii, pia ni kwa sababu ya wimbo wake wenye uliozua utata nchini Rwanda, Igisobanuro cy'urupfu (Maelezo ya kifo kwa Kiswahili). Hiyo ndiyo maana ya Tuzo ya Vaclav Havel. Kulingana na taarifa ya Wakfu wa Haki za Binadamu (Human Right Foundation) , "Kizito Mihigo alionesha ujasiri katika wimbo wake wa mwaka 2014 " ambao aliutunga kuwafariji "wale waliouawa na vikosi vya RPF baada ya mauaji ya kimbari ya waka 1994".

Hata hivyo utawala wa Rwanda ulipiga marufuku wimbo huo ambao unapingana na historia rasmi," Wakfu wa Haki za Binadamu (Human Right Foundation) imekumbusha.

Mara tu baadaye, Kizito Mihigo alikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 kwa "kula njama dhidi ya serikali". Aliachiliwa baada ya miaka minne. Shirika lake halikuweza tena kufanya shughuli zake. Kizito Mihigo alifariki dunia katika mazingira tatanishi akiwa katika jela Februari 17, 2020 baada ya kukamatwa akitaka kuitoroka nchini. Seikali ya Kigali inaendelea kudai kuwa alijiua.

Bwana Kizito ambaye alifariki ndani ya seli ya polisi mjini Kigali mwezi Februari, ni mtu wa kwanza kupewa tuzo hiyo akiwa hayupo duniani tangu ilipozinduliwa mwaka 2012.